Dec 24, 2020 12:31 UTC
  • Mfalme wa Morocco aunga mkono kuanzishwa mazungumzo ya mapatano na utawala wa Kizayuni

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco amefichua kuwa, mazungumzo ya kuanzisha uhusiano kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni yameanza kwa uungaji mkono wa Mfalme wa nchi hiyo.

Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya Kizayuni ya A-24, Nasser Bourita Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco amefichua kuwa, mazungumzo kwa ajili ya kuanzisha uhusiano kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel yalianza tangu mwaka 2018 na muungaji mkono wa mazungumzo hayo ni Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco. 

Mfalme wa Sita wa Morocco  

Yapata karibu wiki mbili sasa ambapo Morocco na utawala wa Kizayuni zimeanzisha uhusiano wa kawaida kati yao kufuatia mashinikizo ya kila upande ya rais wa Marekani, Donald Trump.

Mapatano yaliyofikiwa kati ya nchi kadhaa za Kiarabu na utawala haramu wa Kizayuni ya kuanzisha uhusiano wa kawaida yameughadhibisha pakubwa Ulimwengu wa Kiislamu.

Rais Ismail Omar Gulleh wa Djibouti pia amelaani hatua ya baadhi ya tawala za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Tags