Aug 03, 2021 16:44 UTC
  • William Ruto
    William Ruto

Kuzuiliwa kwa Naibu Rais wa Kenya, William Ruto Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi kusafiri kwenda Uganda kumewakera wandani wake.

Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto alipanga kuzuru nchi hiyo jirani jana lakini maafisa wa Idara ya Uhamiaji walimzuilia wakidai kuwa anahitajia kupata idhini ya kutoka nje ya nchi kutoka Ofisi ya Rais.

Baadhi ya wafuasi wake wanasema hatua hiyo ni kampeni inayoungwa mkono na Serikali kwa ajili ya kumdhalilisha.

Hiyo ingekuwa safari ya pili ya Ruto kwenda Kampala, Uganda katika kipindi cha mwezi mmoja. Mwezi uliopita pia Ruto alifanya safari Uganda kwa shughuli ambazo hazikuelezwa.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Wilson jijini Nairobi kwa ajili ya kupanda ndege, Ruto aliambiwa kwamba anapaswa kupata idhini kutoka kwa Mkuu wa Utumishi wa Umma. Kisha aliamriwa kusubiri saa tano kabla ya safari yake kufutwa.

Baada ya kuzuiwa kuondoka nchini, Ruto alisema katika ujumbe wa Twetter kwamba "ni sawa tu, tumwachie Mungu".

William Ruto

Mwandani mkuu wa kisiasa wa William Ruto, seneta wa Elgeyo- Marakwet Kipchumba Murkomen amefananisha tukio hilo na mihangaiko iliyompata Dkt Miguna Miguna.

“Dkt Ruto hajawahi kuhitaji idhini yoyote ya kusafiri nje ya nchi. Hakuna sheria yoyote inayomlazimisha kupewa ruhusa akitaka kufanya ziara ya kibinafsi. Kilichofanyika leo ni kumkosea heshima Naibu Rais,” alisema Bw Murkomen katika akaunti yake ya Twitter.

Inasemekana kuwa Ruto anajitayarisha kwa ajili ya kugombe kiti cha rais wa Kenya mwaka 2022. 

Tags