Jan 02, 2021 08:08 UTC
  • Hajj Qassem Soleimani; mhimimili wa muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni

Alfajiri Januari Tatu unatimia mwaka wa kwanza wa kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Hajj Qassem Suleimani. Mhimili wa muqawama unakumbushia shahid huyo mkubwa na utawala wa Kizayuni pia umefurahishwa kwa kuuliwa kamanda huyo wa muqawama. Swali muhimu hapa ni hili kuwa Kamanda Suleimani alitoa huduma gani kwa muqawama ambayo imeughadhibisha utawala wa Kizayuni?

Kazi iliyofanywa na Hajj Qassem Soleimani inaweza kubainishwa katika nukta tofauti. Jambo la kwanza ni kuwa Hajj Qassem alikuwa mhimili wa mshikamano na umoja wa muqawama. Moja ya stratejia muhimu sana za Uzayuni wa kimataifa ni kuzusha migawanyiko na hitilafu kati ya nchi za Kiislamu; na kuhusiana na mhimili wa muqawama pia stratejia hizo zina lengo la kuzuia umoja na mshikamamo baina ya makundi mbalimbali. Mshikamano huo na umoja baada ya kupita muda umepelekea kuimarika nafasi ya mhimili wa muqawama na kubadilisha pia mlingano wa nguvu.  

Kamanda shahid Hajj Qassem Suleimani 

Jambo jingine ni kuwa, ngano ya kutowezekana na kutoshindika utawala wa Kizayuni ilivunjwa waziwazi mwaka 2006. Hadi kufikia mwaka 2006 utawala wa Kizayuni ulikuwa ukipata ushindi kwa miongo yote katika vita kati yake na nchi za Kiarabu, hata hivyo vita vya siku 33  vilihitimisha hiyo ngano ya kutoshindika vitani Israel. Shahid Suleimani alikuwa na nafasi kuu na athirifu katika uwanja huo. Nafasi hiyo ilitekelezwa katika kalibu ya kutomuhofia adui, kuongoza medani ya vita na kuingiza ari ya imani miongoni mwa wapiganaji ili kuibuka na ushindi. Al Haj Hussein al Khalil Naibu wa Kisiasa wa Katibu Mkuu wa harakakati ya Hizbullah ya Lebanon anasema kuhusiana na na nafasi ya shahid Hajj Qassem Suleimani katika vita vya siku 33 kwamba: Hajj Qassem alikuwa akivifuatilia vita kutokea ndani ya medani na ndani ya Lebanon. 

Jambo la tatu ni kuwa, alisaidia kuimarisha nguvu ya kujibu mashambulizi ya mhimili wa muqawama. Kabla ya kujiri vita vya siku 33 mwaka 2006 ambapo mhimili wa muqawama haukuwa vizuri katika upande wa zana za kijeshi lakini pole pole hali hiyo ilibadilika. Makombora ya muqawama leo hii yanaweza kupiga kila nukta ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kuhusiana na hilo, Ziyad al Nakhalah Katibu Mkuu wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesifu nafasi ya Hajj Qassem katika kutoa mchango na kusaidia muqawama wa Palestina na kueleza kuwa: Hajj Qassem alikuwa kigezo cha kuwafunza Wapalestina kuunda silaha; na sasa muqawama wa Palestina umepiga hatua pia katika kujitengeneza silaha.  

Ziyad al Nakhalah, Katibu Mkuu wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina

Hizo ni baadhi tu ya mchango mkubwa wa kimkakati aliotoa Hajj Qassem Suleimani kwa kambi ya muqawama. Muda wa vita kati ya mhimili wa muqawama na utawala wa Kizayuni umepungua ikiwa ni natija ya huduma hizo ambazo bila shaka zimetekelezwa kwa msaada na ushirikiano wa makamanda wengine wa muqawama na shakhsia watajika kama Imad Mughniya, Abu Mahdi al Muhandes na wengineo. Tangu kujiri vita vya siku 33 mwaka 2006 hadi sasa utawala wa Kizayuni haujaanzisha hata vita moja dhidi ya Hizbullah ya Lebanon kwa sababu inafahamu vyema nguvu na uwezo wa kujibu mashambulizi wa Hizbullah. Vita vya utawala wa Kizayuni na Wapalestina vimepungua hadi siku mbili; ambapo vita vya mwisho kujiri kati ya pande hizo vilikuwa mwaka 2019 na baada ya kupita siku mbili  utawala huo ulilazimika kukubali usitishaji vita.   

Mchango mwingine mkubwa uliotolea na Hajj Qassem Suleimani kwa mhimili wa muqawama ni mapambano dhidi ya ugaidi katika muongo mmoja wa karibuni. Mhimili wa Waarabu, Waebrania na Magharibi uliyatumia makundi ya kigaidi ili kuipindua serikali halali ya Syria au kuigawa vipande  ardhi na kuanzisha utawala wa genge la kigaidi la Daesh huko Iraq. Bila ya shaka kufeli mhimili huo kutimiza malengo yake ni matokeo ya nafasi isiyoweza kubadilishwa na Hajj Qassem Suleimani katika kupambana na ugaidi. Sayyid Hassan Nasrullah Katibu, Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon anasema kuhusu hilo kwamba: makamanda wa Iraq wanasema kuwa Hajj Qassem siku zote alikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya wakufurishaji wa kundi la Daesh; na alikuwa bega kwa bega na bega na wanajeshi wa Iraq na Syria kuwafurusha magaidi hao.  

Genge la ukufurishaji la Daesh (ISIS)

Mchango huo mkubwa umeulazimisha utawala wa Kizayuni na Marekani kuwa na hasira na ghadhabu na kamanda mkubwa wa mhimili wa muqawama Hajj Qassem Suleimani; na hivyo kuamua kutenda jinai kubwa ya kumuuwa kigaidi kamanda huyo mkubwa wa muqawama.

Tags