May 19, 2021 08:11 UTC
  • Hatami: Intifadha imeigeuza kuwa jinamizi ndoto ya Wazayuni ya 'kuanzia Nile hadi Euphrates'

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kwa kuivuka Intifadha ya kupambana kwa mawe na kuingia kwenye Intifadha ya kupambana kwa makombora, wananchi mashujaa wa Palestina wameigeuza ndoto ya Wazayuni ya kutawala kuanzia Mto Nile hadi Mto Euphrates kuwa jinamizi la kupigania kuilinda kambi ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa Iisrael.

Brigedia Jenerali Amir Hatami ameyasema hayo leo katika mazungumzo aliyofanya hapa mjini Tehran na Jamaluddin Ibrahim Shuaib, Naibu Waziri wa Biashara za Ndani na Jamal al Umr, Naibu Waziri wa Viwanda wa Syria.

Sambamba na kulaani jinai zisizosameheka za utawala ghasibu wa Kizayuni za kuwaua shahidi hata watoto wadogo na wanwake wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza, Hatami amesema, kwa ilhamu waliyopata kutokana na muqawama na kusimama kidete wananchi wa Syria katika vita na makundi ya ukufurishaji na kigaidi yaliyokuwa yakiungwa mkono na mfumo wa ubeberu na utawala wa Kizayuni, wananchi mashujaa wa Palestiina wameugongesha mwamba utawala ghasibu na haramu wa Israel kwa kuufanya ushindwe kufikia malengo yake maovu.

Wanamuqawama wa Palestina, ambao sasa wanapambana na utawala wa Kizayuni kwa kutumia silaha nzito, zikiwemo za makombora

Katika mazungumzo hayo, Brigedia Jenerali Amir Hatami ameashiria pia nafasi na umuhimu wa kistratejia wa Syria katika mhimili wa muqawama na akaeleza kwamba kwa uwezo wake wote, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuwa bega kwa bega na wananchi na serikali ya Syria katika kusaidia kulinda umoja wa ardhi ya nchi hiyo na kushiriki kwenye ujenzi na ukarabati wake.../

Tags