Jul 31, 2021 02:40 UTC
  • Iran yasikitishwa na moto mkubwa wa misituni ulioikumba Uturuki

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza masikitiko yake kufuatia moto mkubwa unaoendelea kuteketeza misitu nchini Uturuki.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Saeed Khatibzadeh jana Ijumaa alieleza masikitiko yake kufuatia moto mkubwa ulioathiri misitu ya mikoa ya kusini mwa Uturuki na kusababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu iko pamoja na serikali na taifa rafiki na ndugu la Uturuki na ametoa mkono wa pole kwa familia za watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.

Khatibzadeh amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuisaidia serikali ya wananchi wa Uturuki katika kipindi hiki cha maafa.

Sehemu kubwa ya maeneo ya misitu katika mikoa Adana, Merisin na Othmania imeteketea kwa moto ulioanza Jumatano wiki hii katika misitu ya Manavgat katika viunga vya Antalia nchini Uturuki. 

Tags