Aug 02, 2021 04:11 UTC
  • Rais Rouhani: Uzinduzi wa miradi ni mwiba wa kooni kwa waliokuwa wakila njama dhidi ya Iran

Rais Hassan Rouhani amesema, kuzinduliwa kwa miradi ni mwiba wa kooni kwa waliokuwa wakipanga njama mbalimbali dhidi ya Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyasema hayo jana katika hafla ya uzinduzi wa miradi ya kitaifa ya wizara za mafuta, ushirika, kazi na ustawi wa jamii pamoja na shirika la nishati ya atomiki na akaeleza kwamba, nchi hii daima imo katika hali ya ujenzi na uzinduzi na watu wote wanafanya hima na bidii kwa ajili ya hilo.

Rais Rouhani ameongeza kuwa, licha ya kuwepo virusi vya corona; na katika upande mwingine vita vya kiuchumi, lakini kulikuwa na umuhimu mkubwa wa kutoa jibu kwa dunia; na tab'an jibu kuu lilikuwa ni kusimama imara na kuonyesha muqawama wananchi.

Vinu vya usafishaji mafuta vya Iran

Akihutubia katika uzinduzi wa miradi hiyo uliofanyika kwa kutumia mawasiliano ya intaneti na kwa njia ya video, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alibainisha: "Leo tumezindua gati zote za baharini na zinazohusiana na awamu 27 za Pars ya Kusini, ambayo ni miradi mikubwa zaidi ya kiuchumi katika historia ya Iran."

Rais Rouhani aidha amesema, wakati mtu anapowasili Asaluye, kusini mwa Iran anakutana na ulimwengu mkubwa wa karakhana, vinu vya usafishaji mafuta pamoja na gati za nje na ndani ya maji, ambazo ni matunda ya kazi kubwa ya uhandisi iliyofanywa nchini.../

Tags