Aug 03, 2021 02:28 UTC
  • Khatibzadeh: Tuhuma za Uingereza na Marekani dhidi ya Iran hazina msingi, ni za kichochezi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezitaja tuhuma zisizo na msingi zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza dhidi ya Iran ambazo zimekaririwa tena na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kuwa zinakinzana, ni za uwongo na za kichochezi.

Saeed Khatibzadeh  Khatibzadeh amelaani vikali tuhuma hizo na kusema kuwa taarifa hizo zilizoratibiwa zimejaa masuala yenye kukinzana kiasi kwamba nchi hizo, awali na bila ya kuwasilisha nyaraka na ushahidi wowote, zilitoa tuhuma za uwongo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kisha zikaanza kudai kuwa tuhuma hizo yumkini zikawa za kweli. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  amesema kuwa, Tehran inaunga mkono safari za meli za amani na zisizo na madhara katika Ghuba ya Uajemi na katika maji ya kimataifa; na siku zote iko tayari kushiriki katika jitihada za kudhamini usalama wa meli katika eneo hilo.

Ghuba ya Uajemi 

Iran inaamini kuwa kuwepo vikosi vya majeshi ya nchi ajinabi katika maji ya Ghuba ya Uajemi na katika nchi za pambizoni mwa eneo hilo kunavuruga amani na usalama wa eneo hilo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa inasikitisha kuona nchi hizo zimenyamaza kimya mkabala na mashambulizi ya kigaidi na uharibu unaofanywa dhidi ya meli za biashara za Iran katika Bahari Nyekundu na katika maji ya kimataifa.