May 21, 2021 12:19 UTC
  • Baada ya kushindwa Ghaza, sasa Wazayuni walana wao kwa wao

Baada ya kushindwa katika vita vya siku 11 baina yao na wanamapambano wa Palestina, sasa wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamenza kupapurana wao kwa wao.

Wabunge wa utawala wa Kizayuni wamelaani udhalili iliotumbukia Israel kwa kukubalishwa kusimamisha vita na wanamapambano wa Palestina na wamesema kuwa, hiyo ni fedheha kwa utawala huo.

Mbunge Ayelet Shaked wa utawala wa Kizayuni amesema kuwa, kulazimishwa utawala wa Kizayuni kusimamisha vita bila ya masharti yoyote ni aibu na fedheha kwa Israel. 

Mbunge huyo Mzayuni amemlaumu vikali sana waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu kwa kushindwa hata kuwakomboa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na wanamapambano wa Palestina huko Ghaza.

Mbunge mwingine wa Israel, Gideon Sa'ar kutoka chama cha "Matumaini Mapya" amesema, kulazimika utawala wa Kizayuni kusimamisha vita bila ya kupata mafanikio yoyote, ni kashfa na aibu kwa Israel. Mbunge mwingine Mzayuni amelalamika kuwa, kitendo cha Israel cha kukubali kusimamisha vita kwa sura hii ya aibu na udhalili ni hatari sana kwa utawala wa Kizayuni na kitauweka utawala huo katika wakati mgumu sana.

Muqawama wa wanamapambano wa Palestina

Wananchi wa maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina walimiminika mitaani na barabarani kushangiria ushindi, sekunde chache baada ya kutangazwa kuanza utekelezaji wa kusimamishwa vita baina ya utawala wa Kizayuni wa Israel na wanamuqawama wa Palestina, saa nane kamili usiku kwa majira ya eneo hilo.

Baada ya siku 11 za hujuma na mashambulio ya kijeshi ya utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel, hatimaye jana saa nane usiku utawala huo ulianza kutekeleza usimamishaji vita kwa kuhofia vipigo zaidi vya makombora na maroketi ya wanamapambano wa Palestina.

Tags