May 23, 2021 02:50 UTC
  • Waandishi habari 170 walijeruhiwa katika vita ya Israel dhidi ya Gaza

Mwenyekiiti wa Jumuiya ya Waandiihi Habari huko Palestina amesema kuwa waandishi wa habari wanaokaribia 170 walijeruhiwa katika mashambulizi ya karibuni ya Israel na kwamba jumuiya hiyo itawasilisha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kuhusiana na suala hilo.

Naser Abu Bakr amesema kuwa mashambulizii ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Gaza yamejeruhi karibu waandishi habari 170. Ameongeza kuwa, ofisi 33 za mashirika na vyombo vya habari zimeharibiwa kwa mashambulizi na mabomu ya utawala ghasibu wa Israel.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi Habari huko Palestina amesema kuwa, jumuiya hiyo ikishirikiana na waandishi habari wa kimataifa inatayarisha hati ya mashtaka kuhusu jinai na uhalifu uliofanywa na Israel dhidi ya waandishi wa habari na baadaye itaiwasilisha katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai. 

Ijumaa iliyopita pia Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mohammad Shtayyeh alisema kuwa jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni katika vita vya siku 11 vilivyomalizika usiku wa kuamkia Ijumaa ikiwa ni pamoja na kuua kikatili wanawake na watoto wadogo wa Kipalestina, zitafunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). 

Mtoto wa Kipalestina akimuaga ndugu yakke aliyeuawa katika shambulizi la Israel, Gaza

Wapalestina 243 wameuawa na maelfu ya wengine wamejeruhiwa katika mashambulizi ya siku 11 ya Wazayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza. 66 kati ya waliouliwa shahidi walikuwa watoto wadogo. 

Tags