Jul 06, 2021 08:14 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar aelekea Beirut kuchunguza mgogoro wa kuunda serikali ya Lebanon

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar leo anaelekea Beirut mji mkuu wa Lebanon kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo ambapo pande mbili zitachunguza mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini humo kuhusu suala la kuasisi serikali ya Lebanon.

Muhammad bin Abdulrahman Al Thani katika safari yake hiyo ya siku moja huko Lebanon atakuwa na mazungumzo na Rais Michel Aoun wa nchi hiyo, Saad Hariri Waziri Mkuu aliyepewa jukumu ya kuunda serikali, Hassan Diab Waziri Mkuu anayeongoza masuala ya Lebanon, Spika wa Bunge Nabih Beri na Joseph Aoun Kamanda wa Jeshi la nchi hiyo.  

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Al Thani ameelekea Beirut katika jitihada za Doha za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa wa Lebanon.  

Katika mazungumzo aliyofanya na Saad Hariri mwezi Februari huko Qatar, Amir wa Qatar Tamim bin Hamad Al Thani alizihimiza pande za kisiasa huko Lebanon kutoa kipaumbele kwa maslahi ya kitaifa na kuharakisha serikali mpya inaundwa nchini Lebanon. 

Katika mazungumzo hayo, Hariri alizungumzia matukio muhimu zaidi ya Lebanon na juhudi zinazohusiana na uundaji wa serikali mpya. 

Lebanon imetumbukia katika mgogoro wa kisiasa baada ya kutokea mripuko mkubwa katika bandari ya Beirut. Mlipuko mkubwa ulitokea katika bandari hiyo tarehe Nne Agosti mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 190 na kujeruhi wengine 6,500. 

Mlipuko mkubwa katika bandari ya Beirut mwaka jana 2020 

 

Tags