Aug 01, 2021 05:28 UTC
  • HAMAS: Marekani inaipa baraka Israel za kuendeleza mauaji yake dhidi ya Wapalestina

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, uamuzi waserikali ya Marekani wa kuupatia silaha mpya utawala haramu wa Israel maana yake ni kuupa baraka utawala huo ghasibu za kuendeleza hujuma na mashambulio yake dhidi ya wananchi wa Palestina.

Hazim Qassim amelaani vikali, himaya na uungaji mkono wa serikali ya Marekani kwa siasa za utawala ghasibu wa Israel na kusema kwamba, inaonekana kuwa, Washington inataka kuwafungulia njia Wazayuni ya kuendeleza hujuma na vitendo vyao vya kigaidi dhidi ya taifa madhulumu la Palestina kwa kuupatia silaha mpya utawala huo haramu.

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, kitendo cha serikali ya Marekani cha kuendelea kuwapatia silaha Wazayuni wavamizi kinapelekea kushadidi mizozo na machafuko katika eneo la Asia Magharibi na wakati huo huo kuongezeka mauaji ya wavamizi.

Hazim Qassim msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS

 

Kadhalikka Hazim Qassim msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, mlolongo wa himaya na uungaji mkono wa kifedha na kisilaha wa Marekani kwa siasa za kivamizi za Wazayuni maghasibu umeifanya Washinghton iwe mshirika wa jinai zinazofanywa kila uchao na Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.

Wakati huo huo, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema mashambulio yaliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku 11 dhidi ya Ukanda wa Gaza yalifikia kiwango cha jinai za kivita.

Tags