Aug 01, 2021 08:09 UTC
  • Judoka mwingine, raia wa Lebanon akataa kupambana na Mzayuni

Mwanajudo wa Lebanon, Abdullah Miniato ametangaza kujiondoa katika mashindano ya kimataifa ya mchezo wa mixed martial arts (MMA) huko mjini Sophia, Bulgaria, na kwa utaratibu huo anakuwa judoka wa tatu kukwepa kuvaana na hasimu kutoka utawala haramu wa Israel katika mashindano ya Olimpiki ya Tokyo 2020.

Judoka huyo pamoja na mkufunzi wake Muhammad Al-Gharbi, wametangaza kujiondoa kwenye mpambano huo wa kimataifa, baada ya droo iiyochezeshwa jana Jumamosi kumpanga barobaro huyo achuane na hasimu Mzayuni.

Hatua hii ni mwendelezo wa upinzani dhidi ya utawala haramu wa Israel ambao umeendelea kupata pigo katika mashindano yanayoendelea ya Olimpiki ya Tokyo 2020 nchini Japan. Hii ni baada ya wanajudo wengine wawili kutoka Algeria na Sudan kukataa kupambana na washindani wao kutoka Israel. Majudoka hao ni Mohamed Abdalrasool wa Sudan na Fat'hi Nourin wa Algeria.

Gazeti la Kiebrania la Yediot Ahronot liliandika katika toleo lake la hivi karibuni kuwa, historia imethibitisha kuwa ukweli hauwezi kubadilishwa na kwamba mapatano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu yako makaratasini tu, lakini katika mazingira halisi ya mahusiano ya kiutu, wanamichezo wa nchi za Kiarabu wamethibitisha kuwa, kwa mtazamo wao, hakuna nchi inayoitwa Israel.

Fathi Nourin wa Algeria akiwa na bendera ya Palestina

Aprili mwaka jana, Shirikisho la Judo Duniani (IJF) lililipiga marufuku ya miaka minne Shirikisho la Judo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIJF) baada ya Tehran kulitaka lisiwapange wanamichezo wake mkabala na mahasimu wa Israel.

Huku hayo yakijiri, IJF imeipongeza Saudi Arabia baada ya mwanamichezo wa kike wa nchi hiyo ya Kiarabu kukubali kupambana na Mzayuni katika mashindano ya Olimpiki ya Tokyo.

Tags