Aug 02, 2021 08:09 UTC
  • Ismail Hania achaguliwa tena kuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imemchagua tena Ismail Hania kuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo ya muqawama.

Duru zilizoko karibu na Hamas zimeripoti kuwa, Ismail Hania amechaguliwa tena kwa mara ya pili mtawalia kuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina.

Hivyo basi Ismail Hania ataandelea kuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS kwa miaka mingine minne yaani hadi mwaka 2025.

Ismail Hania alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017 kuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, makubaliano ya kuongeza muda wa uongozi wa Ismail Hania kwa miaka mingine minne umepasishwa baada ya kukosekana mgombea wa kushindana naye hasa baada ya Khalid Mash'al aliyewahi kuwa kuongoza nafasi hiyo kukataa kushiriki kinyang'anyiro hicho.

Wanamapambano wa Hamas

 

Katika upande mwingine, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS  imepongeza misimamo ya Algeria katika kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Taarifa ya Hamas imesisitiza kuwa, harakati hiyo inathimi

ni na kupongeza misimamo ya serikali ya Algeria na hatua yake ya kuanzisha kampeni ya kupinga hatua ya Umoja wa Afrika ya kuiteua Israel kkuwa mwanachama mtazamaji wa AU.

Hamas imezitaka nchi zote za Kiarabuu na Kiislamu kkuchukua hatua kama ya Algeria ya kupinga kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.