Aug 03, 2021 10:47 UTC
  • Stéphane Dujarric
    Stéphane Dujarric

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa ujenzi unaofanywa na Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ni kinyume cha sheria.

Stéphane Dujarric amewaambia waandishi habari kwamba, Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu kesi ya eneo la Sheikh Jarrah inayoendelea katika mahakama ya Israel ambayo hukumu yake imepangwa kutolewa wiki hii.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, msimamo wa siku zote wa UN ni kwamba, shughuli zote za ujenzi wa vitongoji vya walowezi ikiwa ni pamoja na kuwafukuza Wapalestina na kuharibu nyumba zao, vinakiuka sheria za kimataifa.

Awali Ripota Maalumu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa huko Palestina alikuwa amesema kuwa nzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza unakiuka sheria za kimataifa.

Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, Palestina

Michael Lynk amesema kuwa, nchi za Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya pia zimekiuka sheria za kimataifa kwa kuipa Israel silaha zinazotumika kushambulia watu wa Gaza na Syria. 

Amesema azimio nambari 1998 pia linasisitiza kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina ni sawa na kukanyaga na kukiuka haki za binadamu.