Nov 28, 2020 03:25 UTC
  • Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia
    Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia

Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia ameyatuhumu madola ya Magharibi mwamba, yanaingilia masuala ya ndani ya Russia na Belarus na kuyalaumu pia kwa kutekeleza vikwazo vya upande mmoja na kuwachochea wananchi wa mataifa hayo ili waanzishe vurugu na machafuko.

Lavrov amesema kuwa, madola ya Magharibi yamekuwa yakitumia teknolojia kwa ajili ya kuratibu uasi wa uma nchini Russia na Belarus huku diplomasia na vyombo vyao vya habari navyo vikitupatia makataa. Madola hayo yamekuwa yakifanya mambo bila kificho na kufanya hima ya kuwa na taathira katika mambo yetu ya ndani.

Matamshi ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia yanaashiria njama mtawalia za Magharibi zikiongozwa na Marekani ambazo zimeshuhudiwa baada ya vita baridi na lengo lake ni kuidhoofisha Moscow, na wakati huo huo kuleta mageuzi ya kisiasa kwa kutumia njia ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Sergey Kogmiyakin mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa Russia anasema: Kinyume na matamshi na nara za kipropaganda kuhusiana na uhuru, demokrasia na haki za binadamu, lengo kuu la mfumo wa kibeberu duniani ni kujitanua. Kudhibiti masoko mapya na kuziondoa madarakani tawala ambazo hazikubaliai na mfumo huo ndio sharti la kubakia kwa mfumo huo.

 

Katika kipindi cha baada ya Vita Baridi, Russia daima imeandamwa na utendaji wa madola ya Magharibi wa kuingilia masuala yake ya ndani katika fremu ya mapinduzi laini. Suala hilo lilishadidi zaidi baada ya kuibuka mgogoro wa Ukraine mwaka 2014 na kupamba moto makabiliano ya Mosco na Jumuiya ya Kijeshi ya Nchi za Magharibi NATO mashariki mwa Ulaya na Marekani na Ulaya kuchukua hatua ya kuiwekea Russia vikwazo mbalimbali.

Kwa mtazamo wa viongozi wa Russia ni kuwa, madola ya Magharibi yana mkono wao nyuma ya pazi la malalamiko ya wananchi huko Russia na Belarus, ambapo madola hayo yanafanya njama za kuanzisha uasi wa uma na mapinduzi ya mahameli na badala yake waziweke madarakani katika nchi mbili hizo tawala ambazo zitakuwa na muelekeo wa Kimagharibi.

Filihali viongozi wa Moscow wana wasiwasi wa kutokea mapinduzi laini katika nchi za Jumuiya ya Madola, Commonwealth. Katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa kushadidi hatua za madola ya Magharibi hususan Marekani za kuingilia masuala ya ndani ya Russia kwa shabaha ya kuzusha machafuko, kuongeza malalamiko ya wananchi na hatimaye kuandaa mazingira ya kutokea mapinduzi ya mahameli nchini Russia.

Mvutano wa Russia na Marekani umeongezeka mno katika kipindi cha utawala Donald Trump

 

Moja ya hatua muhimu katika uwanja huo ni kuongezwa misaada ya kifedha na uungaji mkono wa kila upande wa kihabari kwa wapinzani sambamba na kuzusha  anga hasi ndani ya Russia. Baada ya kushindwa wapinzani wa Russia katika juhudi zao za kuidhoofisha serikali ya Moscow, kumeshuhudiwa kushadidi mashinikizo na vikwazo vya Marekani ikishirikiana na Umoja wa Ulaya kupitia sheria ya CAATSA ambapo lengo hasa ni kushadidisha mashinikizo dhidi ya serikali ya Moscow na wakati huo huo kuibua malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali hiyo.

Sergey Lavrov, sambamba na kuashiria utendaji wa kuhujumu na kushambulia wa Ulaya na Marekani dhidi ya Moscow amesema: Madola ya Magharibi hayafanyi mambo kwa kuheshimu sheria, bali yamekuwa yakitekeleza vikwazo vya upande mmoja na hayatoi nyaraka na ushahidi wowote wa kuthibitisha madai yao.

Wakati huo huo, kwa sasa Moscow ina wasiwasi na juhudi mtawalia za Magharibi na Marekani na katika hatua ya baadaye ina wasiwasi na hatua za Umoja wa Ulaya za kutaka kuanzisha mapinduzi ya mahameli katika nchi za kando kando na Russia.

Rais Alexander Lukashenko wa Belarus

 

Hatua hizo zimewahi kufanywa katika nchi kama Georgia, Ukraine na Kyrgyzstan na wakati wa kujiri machafuko ya kisiasa pia hivi karibuni huko Belarus, madola ya Magharibi yalikuwa yakifuatilia suala la kutekeleza hatua kama hizo katika nchi hiyo ya mashariki mwa Ulaya ambayo inahesabiwa kuwa muitifaki mkuu wa Russia.

Serikali ya Russia inaona kuwa, madola ya Magharibi hususan Umoja wa Ulaya na Marekani yana mpango unaofanana ambao wanakusudia kuutekeleza nchini Belarus kupitia kushadidisha mashinikizo ya kisiasa na kuwaunga mkono waziwazi wapinzani sambamba na kutekeleza vikwazo vipana dhidi ya viongozi wa ngazi za juu wa nchi hiyo.

Tags