Jan 04, 2021 07:50 UTC
  • Ripota wa UN: Mauaji ya Kamanda Soleimani ni kinyume na sheria za kimataifa

Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, mauaji ya kigaidi ya shahid Hajj Qassem Soleimani ni kinyume na sheria za kimataifa na kuongeza kuwa, mauaji hayo yaliyofanywa na Marekani ni uvunjaji wa haki ya kujitawala ardhi ya Iraq.

Bi Agnes Callamard amesema hayo leo katika mtandao wa kijamii wa Twitter na kwa mara nyingine amelaani mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani na kusisitiza tena kwamba mauaji hayo yalifanywa kinyume cha sheria za kimataifa.

Kabla ya hapo pia, yaani tarehe 9 Julai 2020, Bi Agnes aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Marekani imeshindwa kutoa ushahidi wa kuthibitisha kwamba Jenerali Soleimani alikuwa tishio kwa roho za Wamarekani na kwamba kumuua kigaidi kiongozi huo wa ngazi za juu wa Iran tena katika nchi nyingine, kunakinzana na sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa.

Bi Agnes Callamard

 

Aidha wakati alipohojiwa na shirika la habari la Reuters, ripota huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa alisema, madai ya Marekani kwamba Luteni Jenerali Soleimani alikuwa tishio kwa usalama wa roho za Wamarekani huko Iraq hayana msingi wowote na hivyo kumuua jenerali huyo kulikanyaga sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa Mataifa.

Shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, aliuliwa kidhulma katika shambulio la kuvizia la anga lililofanywa na wanajeshi magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq, tarehe 3 Januari, 2020 akiwa uraiani tena akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq, lakini Wamarekani hawakuheshimu hata protokali za kidiplomasia.

Tags