Feb 18, 2021 07:59 UTC
  • Donald Trump
    Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amevishambulia vikali vyombo vya habari katika mazungumzo yake ya kwanza na vyombo vya habari baada ya kuondoka White House akimtuhumu rais wa sasa wa nchi hiyo, Joe Biden kuwa ana matatizo ya kiakili.

Donald Trump ambaye alikuwa akizungumza na televisheni za Fox news Newsmax na OAN zinazompigia debe na kumuunga mkono, amekariri tena madai yake kuwa kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi wa Marekani uliofanyika mwaka jana.

Vilevile ameutaja mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa unachosha baada ya kuzuiwa kutumia mtandao huo kufuatia hujuma iliyofanywa na wafuasi wake dhidi ya majengo ya Kongresi ya Marekani mwezi uliopita ambapo watu wasiopungua 5 waliuawa katika shambulizi hilo.

Trump amesisitiza kuwa: "Biden ana matatizo ya kiakili na bado naamini kuwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana yalichakachuliwa." Madai hayo ya Trump ya kuibiwa kura katika uchaguzi uliopita ndiyo yaliyowachochea wafuasi wake kuvamia majengo ya Kongresi ya Marekani.

Joe Biden alishinda uchaguzi wa rais wa Marekani kwa kupata kura 306 za wajumbe wa jopo maalumu Electoral College dhidi ya Trump aliyepata kura 232.

Tags