Jun 17, 2021 12:42 UTC
  • UN: Watu milioni moja huko Myanmar wana hali mbaya

Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu milioni moja wana hali mbaya huko Myanmar na wanahitaji misaada ya haraka ya kimataifa.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa, watu milioni moja huko Myanmar wanahitaji msaada kufuatia mapigano kati ya jeshi na makundi ya ndani na pia nchi hiyo kuathiiwa na matatizo ya kiuchumi.  

Wakati huo huo vyombo vya habari leo vimeripoti kuwa, Korea Kaskazini imeupatia Umoja wa Mataifa msaada wa dola laki tatu kwa ajili ya Myanmar. Kwa mujibu wa data za Umoja wa Mataifa, huo ni msaada wa kwanza kutolewa na Pyongyang kwa Myanmar tangu mwaka 2005. 

Aung San Suu- Kyi 

Mwaka 2005  na mwaka mmoja baada ya kutokea maafa ya Tsunami huko Asia ya kusini mashariki, Korea Kaskazini ilitoa dola laki moja na nusu kama msaada kwa Myanmar, Indonesia, India, Thailand, Malaysia, Maldive na Sri Lanka. Aidha Korea Kusini pia iliipatia Myanmar msaada wa dola laki sita hata hivyo nchi hiyo ikasitisha mabadilishano yake na zana za kivita kwa nchi hiyo. 

Jeshi la Myanmar lilichukua madaraka baada ya kuipindua serikali ya Aung San- Suu Kyi kiongozi wa chama cha Umoja wa Kitaifa kwa ajili ya Demokrasia Februari Mosi mwaka huu. Wakati huo huo maandamano makubwa ya wananchi dhidi ya watawala wa kijeshi yanaendelea nchini humo licha ya serikali ya kijeshi kuwakandamiza vikali wananchi wanaondamana. 

Tags