Aug 01, 2021 10:55 UTC
  • John Sopko
    John Sopko

Inspekta Jenerali Maalumu wa Marekani katika Ujenzi Mpya wa Afghanistan amesema kuwa, nchi hiyo haijapata ibra na funzo kutokana na makosa yake katika vita vya Afghanistan.

John Sopko ameashiria maafa yaliyotokana na usimamizi mbaya wa Marekani katika vita vya Afghanistan katika kipindi cha miongo iliyopita na kusema, hakuna dhamana yoyote kwamba Washington haitakariri makosa hayo katika siku zijazo. 

Inspekta Jenerali Maalumu wa Marekani katika Ujenzi Mpya wa Afghanistan ambaye alikuwa akitoa ripoti kwenye Baraza la Kongresi amewaambia wabunge hao wa Marekani kwamba: "Msiamini mnayoambiwa na majenerali wa jeshi, mabalozi na maafisa wa serikali wanaodai kwamba makosa hayo hayatakaririwa."

John Sopko amesema madai haya pia yalitolewa baada ya vita vya Vietnam na baadaye tulishuhudia vita vya Iraq na Afghanistan na kukariri makosa yaleyale. 

Wanajeshi wa Marekani wakiwa kwenye mashamba ya mpopi Afghanistan

Baada ya miaka 20 ya kuikalia kwa mabavu ardhi ya Afghanistan hatimaye Marekani imetangaza kuwa, itawaondoa wanajeshi wake wote nchini humo kufikia tarehe 11 Septemba mwaka huu wa 2021.  

Marekani na washirika wake waliivamia Afghanistan mwaka 2001 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kudhamini usalama nchini humo lakini kinyume chake, hujuma na uvamizi huo umeharibu miundombinu yote ya kiuchumi ya Afghanistan na kuzidisha ukosefu wa amani, ugaidi na uzalishaji wa dawa za kulevya. 

Tags