-
Shambulio la RSF laua watu 8 wa familia moja msikitini Sudan
Jul 02, 2024 02:40Watu wanane wa familia moja wameripotiwa kuuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na wapiganaji wa kundi la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) magharibi mwa Sudan.
-
Malik Agar: Kuporomoka kwa Sudan ni hatari kwa nchi zote za kanda hii
Jul 02, 2024 00:41Malik Agar, Makamu wa Rais wa Baraza la Utawala wa Sudan, ameonya juu ya hatari ya kuporomoka kwa Sudan, ambayo haitakuwa kwa nchi hiyo pekee, bali athari zake mbaya zitaenea katika nchi jirani na kwingineko.
-
IOM: Wahamiaji 303 waliokamatwa Libya wamerejeshwa walikotoka katika kipindi cha wiki moja
Jul 01, 2024 23:29Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) lilitangaza jana Jumatatu kwamba, jumla ya wahamiaji haramu 303 waliokamatwa nchini Libya wamereshwa katika nchi zao za asili kwenye kipindi cha wiki moja iliyopita wakiwemo Wabangladeshi 162.
-
Maseneta wa Kenya wamgomea Rais Ruto mpango wa kupunguza matumizi ya serikali
Jul 01, 2024 07:26Rais William Ruto wa Kenya anakabiliwa na changamoto kubwa katika juhudi zake za kupunguza matumizi ya serikali ili kuziba pengo la bajeti la shilingi bilioni 346 huku maseneta wakiapa kukataa kupunguzwa kwa pesa za mgao wa kaunti.
-
Jeshi la Sudan lakomboa Sinja, mapigano yalazimisha watu 55,000 kukimbia
Jul 01, 2024 06:56Jeshi la Sudan limetangaza kuwa limefanikiwa kudhibiti wa makao makuu ya kitengo cha 17 cha jeshi la nchi kavu, makao makuu ya Brigedia ya 67, na vitongoji vyote vya kusini na mashariki vya mji wa Sinja, makao makuu ya Jimbo la Sennar kusini-mashariki mwa Sudan.
-
Tume: Watu milioni 9.7 wametimiza masharti ya kupiga kura nchini Rwanda
Jul 01, 2024 02:20Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Rwanda imetoa orodha ya mwisho ya wapiga kura, ikionyesha kwamba watu milioni 9.7 wametimiza masharti ya kushiriki katika uchaguzi wa mwezi huu wa Julai wa kuchagua rais na wabunge katika wilaya 30 za Rwanda na Wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi.
-
Jeshi la Sudan lakanusha madai ya RSF ya kuteka makao makuu ya jimbo la Sennar
Jun 30, 2024 22:52Jeshi la Sudan (SAF) jana Jumapili lilikanusha madai kwamba Askari wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wamechukua udhibiti wa mji wa Singa ambao ni makao makuu ya jimbo la Sennar la katikati mwa Sudan.
-
Nchi za Afrika zahimizwa kuharakisha utekelezaji wa AfCFTA
Jun 30, 2024 22:51Nchi za Afrika zimetakiwa kuwasilisha mipango ya utekelezaji na mikakati ya kitaifa ili kuharakisha ufanikishaji wa malengo ya kuanzishwa Eneo Huria la Biashara ya Bara la Afrika (AfCFTA) na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za bara hilo.
-
Watu 18 wauawa katika mashambulizi ya kigaidi jimboni Borno, Nigeria
Jun 30, 2024 07:55Kwa akali watu 18 wamepoteza maisha huku makumi ya wengine wakijeruhiwa kufuatia wimbi la mashambulizi ya kigaidi katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Ghazouani aongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais Mauritania
Jun 30, 2024 03:26Rais Mohamed Ould Cheikh Ghazouani wa Mauritania yupo kifua mbele huku ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika jana Jumamosi ukiendelea.