-
Mahakama yathibitisha kifungo cha maisha kwa waziri mkuu wa zamani wa Burundi
Jun 28, 2024 03:32Mahakama nchini Burundi imethibitisha kifungo cha maisha jela dhidi ya jenerali Alain Guillaume Bunyoni waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
-
Watu 755,000 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula Sudan
Jun 28, 2024 00:22Wataalamu na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wameonya kuwa, mapigano yanayoendelea nchini Sudan baina ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF yatapelekea watu 755,000 kuwajihiwa na baa la njaa na uhaba mkubwa wa chakula katika miezi michache ijayo.
-
UN: Tumeshtushwa na mauaji dhidi ya waandamanaji Kenya
Jun 27, 2024 23:50Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa kwake na maandamano ya ghasia ya kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 nchini Kenya, yaliyopelekea makumi ya watu kuuawa.
-
Waandamanaji Kenya wamtaka Rais Ruto ajiuzulu licha ya kuurejesha muswada wa fedha bungeni
Jun 27, 2024 09:12Waandamanaji Kenya wanamtaka Rais wa nchi hiyo William Ruto ajiuzulu licha ya uamuzi wake wa kuuondoa muswada tata wa fedha wa 2024 uliokuwa umedhamiria kuongeza ushuru ili kusaidia kupunguza mzigo wa madeni nchini humo.
-
Misri yaikosoa Israel kwa kuiba misaada ya kibinadamu ya Wapalestina
Jun 26, 2024 23:29Waziri wa Mambo ya Nje ya Misri amekosoa hatua ya utawala haramu wa Israel ya kupora na kuzuia kuingizwa na kusambazwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, kupitia kivuko cha Rafah.
-
Le Monde: RSF inatekeleza sera ya maangamizi ya kila kitu huko el Fasher, Magharibi mwa Sudan
Jun 26, 2024 23:28Gazeti la Le Monde linalochapishwa nchini Ufaransa limeripoti kuwa wapiganaji wa kundi la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wanaoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo, wamezidisha mashambulizi dhidi ya El Fasher, mji wa mwisho wa Darfur ambao bado uko chini ya udhibiti wa jeshi la Sudan linaloongozwa na Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na kwamba kutekwa kwa mji huo kutaiwezesha RSF kudhibiti karibu theluthi moja ya magharibi mwa Sudan.
-
Maandamano ya vijana yamlazimisha Ruto kuweka kando Muswada wa Fedha 2024
Jun 26, 2024 11:35Rais William Ruto wa Kenya amesema kwamba hatatia saini Muswada wa Fedha 2024 kuwa sheria. Ni baada ya maandamano makubwa ya siku kadhaa yaliyofuatiwa na mauaji ya waandamanaji mjini Nairobi jumanne ya jana.
-
Makumi ya askari wauawa katika shambulio la kigaidi Niger
Jun 26, 2024 08:20Askari wasiopungua 20 wa jeshi la Niger wameuauwa katika shambulio la 'muungano wa makundi ya kigaidi' magharibi mwa nchi hiyo.
-
Jeshi la Kenya kuingia mtaani kukabiliana na waandamanaji
Jun 26, 2024 03:54Rais wa Kenya William Ruto ametangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vitaingia mitaani ili kuhakikisha vinalinda usalama wa watu na mali zao dhidi ya waandamanaji wanaofanya kile alichokiita uhalifu.
-
Kikosi cha MONUSCO chaondoka rasmi Kivu Kusini
Jun 26, 2024 03:53Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO hatimaye kimefungasha virago vyake na kuondoka Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.