-
Watu 10 wameuawa Nairobi wakati polisi ilipowafyatulia risasi waandamanaji waliovamia bunge
Jun 25, 2024 23:21Watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa jana Jumanne wakati polisi walipowafyatulia risasi mamia ya waandamanaji waliovamia majengo ya bunge jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, kupinga sheria ya iliyopitishwa na wabunge ya kuongeza ushuru.
-
HRW yataka kutumwa ujumbe wa UN nchini Sudan ili kuwalinda raia
Jun 25, 2024 22:49Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kufanya kazi na Umoja wa Afrika haraka iwezekanavyo ili kutuma ujumbe wa kulinda raia nchini Sudan.
-
Wabunge Kenya walazimika kutorokea kwenye afisi zao, sehemu ya Bunge yateketezwa kwa moto
Jun 25, 2024 10:55Wabunge wa Kenya wamelazimika kukimbilia kwenye afisi zao zilizoko Bunge Towers baada ya waandamanaji wanaopinga ushuru kwenye Muswada wa Fedha 2024 kuvamia majengo ya Bunge.
-
Mamia ya askari polisi wa Kenya watumwa Haiti licha ya ukosoaji
Jun 25, 2024 07:12Askari polisi 400 wa Kenya wameelekea nchini Haiti leo Jumanne kwa ajili ya kwenda kulinda usalama na kurejesha uthabiti katika nchi hiyo ya Caribbean.
-
Kenya yaruhusu kufanyika maandamano kwa masharti
Jun 25, 2024 04:14Kithure Kindiki Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya amewataka vijana wanaoandamana kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 kuimarisha amani na usalama, kutobeba aina yoyote ya silaha kutakiwa kuondoka katika maeneo ya mikusanyiko ifikapo saa kumi na mbili jioni.
-
Rais Ruto: Niko tayari kuwashirikisha vijana katika suala la muswada wa fedha
Jun 24, 2024 22:58Rais wa Kenya William Ruto amesema yuko tayari kuwashirikisha vijana katika juhudi za kulitafutia ufumbuzi suala la muswada wa fedha nchini humo. Msimamo huo wa kiongozi huyo umekuja baada ya kushuhudiwa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa siku kadhaa sasa.
-
Mamia waandamana Senegal wakitaka nchi yao kukata uhusiano wa kidiplomasia na Israel
Jun 24, 2024 22:58Mamia ya wananchi wa Senegal wameandamana na kutoa wito kwa nchi yao kukata uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.
-
Watu 7 wauawa, 100 watekwa nyara kaskazini mwa Nigeria
Jun 24, 2024 06:44Genge moja la wabeba silaha limevamia kijiji kimoja huko kaskazini magharibi mwa Nigeria na kuua watu wasiopungua saba, mbali na kuteka nyara makumi ya wengine.
-
FAO yapata dola milioni 25 za kuboresha usalama wa chakula nchini Somalia
Jun 24, 2024 03:21Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa, limetia saini mradi wa dola milioni 25 kwa ajili ya kuboresha usalama wa chakula nchini Somalia.
-
ANC: Vyama 10 vya kisiasa kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Afrika Kusini
Jun 24, 2024 03:21Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kimetangaza kuwa vyama 10 vya kisiasa vyenye viti Bungeni vimekubali kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na ANC (GNU).