Dec 09, 2023 02:28 UTC
  • Zaidi ya dola bilioni 1.8 kukusanywa ili kusaidia utengenezaji wa chanjo barani Afrika

Taasisi ya Kimataifa ya Muungano wa Chanjo Gavi imetangaza maamuzi kadhaa iliyochukua ambayo yatasaidia nchi zenye kipato cha chini kukabiliana na athari za janga la COVID-19 na kuziwezesha kukabiliana na majanga ya kiafya katika siku zijazo. Maamuzi haya yamechukuliwa katika mkutano wa siku mbili chini ya uwenyeji wa serikali ya Ghana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Accra.

Bodi ya Muungano wa Gavi imeidhinisha kuanzishwa haraka mfumo utakaoharakisha utengenezaji wa chanjo barani Afrika (AVMA) baada ya zaidi ya miezi 18 ya ushirikiano wa karibu kati ya Gavi, Umoja wa Afrika (AU) na CDC Afrika.  

AVMA ni utaratibu wa kiubunifu wa ufadhili unaolenga kuanzisha tasnia endelevu ya utengenezaji wa chanjo barani Afrika inayoweza kuboresha uthabiti wa kanda katika kupambana na magonjwa ya milipuko, maambukizo ya magonjwa mbalimbali na dharura zingine za kiafya na vilevile afya ya soko la kimataifa la chanjo. AVMA iliasisiwa kupitia mchakato mpana wa mashauriano uliojumuisha washirika, wafadhili, viwanda, taasisi za kiraia na shakhsia mbalimbali. 

Janga la Uviko-19 na athari zake kwa dunia

Muungano wa Chanjo Duniani (Gavi) ukiwa  mmoja wa wanunuzi wakubwa wa chanjo umesema kuwa unatuma ujumbe mkubwa kwa masoko ya kimataifa kwamba utasaidia utengenezaji wa chanjo barani Afrika. 

Tags