Dec 09, 2023 02:29 UTC
  • WFP: Karibu watu milioni 3 wameathiriwa na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko Afrika Mashariki

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetahadharisha kuhusu tishio linaloongezeka kwa usalama wa chakula Afrika Mashariki kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi za ukanda huo

Michael Dunford, Mkurugenzi wa Kanda wa WFP Afrika Mashariki alisema jana Ijumaa huko Nairobi nchini Kenya kuwa eneo la Mashariki mwa Afrika linakabiliwa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa kuanzia hali ya ukame na kukumbwa namafuriko, masuala yanayosababisha maafa kwa jamii. 

WFP imeonya kuwa, mafuriko hayo yanarudisha nyuma juhudi changa zinazofanywa na nchi za Afrika Mashariki za kukabiliana na madiliko ya hali ya hewa baada ya baadhi ya nchi kuathiriwa na ukame wa muda mrefu. Karibu watu milioni 3 wameathiriwa na mafuriko Afrika Mashariki huku zaidi ya milioni 1.2 kati yao wakilazimika kuhama makazi yao baada ya mvua zisizokoma. 

Mafuriko Afrika Mashariki 

Somalia, Ethiopia, Kenya na Tanzania zinapambana na matokeo mabaya zaidi ya maafa haya ya kimaumbile huku Sudan, Sudan Kusini, Burundi, na Uganda pia zikihisi athari hizo. Mvua hizo kubwa zinazotarajiwa kuendelea kunyesha hadi mapema 2024, zimeibua wasiwasi kuhusu uwezo wa ukanda huo kushughulikia changamoto zinazoongezeka za kibinadamu.

Tags