Wasomali wengine milioni moja kuathiriwa na ukosefu wa usalama wa chakula kutokana na ukame
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeripoti kuwa Ukame, mzozo na kupanda kwa bei za vyakula vinaweza kusabaisha uhaba na kukosekana usalama wa chakula kwa Wasomali wengine milioni moja katika miezi mingine ijayo.
Jean-Martin Bauer Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula na Uchambuzi wa Lishe wa WFP amesema katika kikao mjini geneva Uswisi kuwa uchanganuzi wa hivi karibuni wa Ainisho la Awamu ya Usalama wa Chakula Iliyounganishwa unaonyesha kuwa watu milioni 3.4 tayari wanakabiliwa na viwango vya njaa au zaidi. Idadi hii inakadiriwa kuongezeka hadi milioni 4.4 kati ya mwezi Aprili na Juni ambapo mvua zitakuwa chini ya wastani, na hivyo kusababisha hali ya ukame,"
Bauer amesema, "njaa inaongeza sasa huko Somalia huku ukame mwingine ukiijongea nchi hiyo."
Mkurugenzi Usalama wa Chakula na Uchambuzi wa Lishe wa WFP ameongeza kuwa: Matokeo ya uchambuzi kuhusu usalama wa chakula yamethibitisha kuwa msimu wa mvua ambao haukutarajiwa kuanzia Oktoba hadi Desemba 2024 ulisababisha mavuno kidogo, kupungua malisho kwa haraka na vyanzo vya maji na kwamba uzalishaji wa chakula mwaka jana ulikuwa chini ya asilimia 45; kiwango ambacho ni chini ya wastani.
Ameongeza kuwa, takriban watoto milioni 1.7 walio chini ya umri wa miaka mitano huko Somalia wanatarajiwa kukabiliwa na utapiamlo mkali kufikia Desemba mwaka huu. Kati ya hao, 466,000 wanakabiliwa na utapiamlo mkali," alisema.