Sheikh Dalhu Abdul Mumin: Mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran ni kitendo cha ugaidi
Imamu wa Waislamu wa Kishia wa eneo la Kaskazini mwa Ghana, Sheikh Dalhu Abdul Mumin amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya Iran na kuyataja kuwa ni "kitendo cha wazi cha kigaidi cha Israel ya Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."
Sheikh Dalhu Abdul Mumin amesema, “Ulimwengu wa Kiislamu uliamshwa na kitendo cha kigaidi cha wazi cha Israel cha Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambacho kilipelekea kuuawa shahidi nyota kadhaa wanaong’ara pamoja na raia wasio na hatia, wanawake na watoto.
Imam Abdul Mumin amelaani vikali vitendo vya uoga vya kigaidi na utawala dhalimu wa Israel Mwanazuoni huyo wa Kishiia nchini Ghana ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kuiwajibisha Israel kwa mashambulizi hayo ya kichokozi.
Na kwa mujibu wake, Insha Allah, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itashinda kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumsambaratisha mwovu mzayuni. Na anaamini na ana imani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (SEPAH) usiku wa kuamkia leo limefanya wimbi jipya la mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya utawala wa Kizayuni, baada ya juzi kuanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa jina la "Ahadi ya Kweli III." Vyombo vya habari duniani vimetangaza kwamba mashambulizi ya jana ya Iran dhidi ya Israel yalikuwa makubwa zaidi kuliko ya juzi Ijumaa.