Rais wa Sudan Kusini amuuzulu mkuu wa majeshi baada ya kuhudumu kwa miezi 7 tu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i128104-rais_wa_sudan_kusini_amuuzulu_mkuu_wa_majeshi_baada_ya_kuhudumu_kwa_miezi_7_tu
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemfuta kazi mkuu wa majeshi baada ya kuhudumu katika wadhifa huo kwa muda wa miezi saba tu na kumtangaza mkuu mpya atakayeshika nafasi hiyo.
(last modified 2025-07-09T04:29:54+00:00 )
Jul 09, 2025 04:24 UTC
  • Rais wa Sudan Kusini amuuzulu mkuu wa majeshi baada ya kuhudumu kwa miezi 7 tu

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemfuta kazi mkuu wa majeshi baada ya kuhudumu katika wadhifa huo kwa muda wa miezi saba tu na kumtangaza mkuu mpya atakayeshika nafasi hiyo.

Akihutubia kupitia redio ya taifa, rais Kiir hakutaja sababu ya kumfuta kazi Paul Nang Majok. Majok amekuwa akihudumu kwenye nafasi hiyo tangu mwezi Desemba mwaka jana. Kupitia tangazo hilo, rais wa Sudan Kusini amemchagua Dau Aturjong kuwa mkuu mpya wa majeshi.

Majok alikuwa anasimamia jeshi wakati wa mapigano na wanamgambo wanaojumuisha zaidi vijana wa kabila la Nuer, na kusababisha mzozo wa kisiasa unaoendelea hivi sasa.

"Kumekuwa na utamaduni kuwa unapoteuliwa, au kuhamishiwa majukumu hupewi sababu za kuteuliwa na hakuna haja ya kupewa sababu unapoachishwa kazi. Ni jambo la kawaida," amesema Lul Ruai Koang, Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.

Sudan Kusini imekuwa katika amani rasmi na makubaliano ya amani tangu mwaka 2018 yaliyohitimisha miaka mitano ya mapigano yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu, lakini machafuko kati ya jamii zinazozozana yamekuwa yakitokea mara kwa mara.../