Mufti wa Libya atangaza kuunga mkono Iran katika vita vya kukabiliana na Israel, Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i137194-mufti_wa_libya_atangaza_kuunga_mkono_iran_katika_vita_vya_kukabiliana_na_israel_marekani
Wakati mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yakiendelea, Mufti Mkuu wa Libya ametangaza kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-03-06T08:38:53+00:00 )
Mar 06, 2026 08:38 UTC
  • Mufti wa Libya Sheikh Sadiq al‑Ghariani
    Mufti wa Libya Sheikh Sadiq al‑Ghariani

Wakati mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yakiendelea, Mufti Mkuu wa Libya ametangaza kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sheikh Sadiq al‑Ghariani amesema vita vya sasa vinavyoelekezwa dhidi ya Iran vinalenga kueneza ukafiri na kupunguza imani ya Kiislamu.

Amesema pia kwamba operesheni ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko ndani ya haki yake halali ya kujilinda dhidi ya uchokozi wa utawala wa Kizayuni.

Amesisitiza kuwa ina haki ya kushambulia vituo vya kijeshi vya adui ili kulinda mamlaka na uhuru wa nchi yake.

Sheikh al‑Ghariani ameongeza kuwa leo Iran iko mstari wa mbele katika kukabiliana na njama hatari ya Kizayuni, akisema kuwa lengo la mpango huo ni kupanua ushawishi wa Wazayuni na kulazimisha ajenda hasimu dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Katika vita hivyo, alisema, hakuna Mwislamu anayepaswa kuwa upande wa maadui au kubaki bila msimamo.

Mwanazuoni huyo mwandamizi wa Kiislamu pia alisisitiza umuhimu wa umoja wa Kiislamu, akisema kuwa Waislamu wanapaswa kuweka kando tofauti zao.