Afrika Kusini yabaini maambukizi ya virusi vya Hanter vinavyohusishwa na meli ya utalii
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i138198-afrika_kusini_yabaini_maambukizi_ya_virusi_vya_hanter_vinavyohusishwa_na_meli_ya_utalii
Afrika Kusini imebaini virusi kwa jina la Hanter aina ya Andes ambavyo hueneza maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu katika watu wawili waliotoka kwenye meli iliyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo. Haya yameelezwa leo bungeni na Waziri wa Afya wa nchi hiyo.
(last modified 2026-05-06T10:38:29+00:00 )
May 06, 2026 10:24 UTC
  • Afrika Kusini yabaini virusi vya Hanter aina ya Andes
    Afrika Kusini yabaini virusi vya Hanter aina ya Andes

Afrika Kusini imebaini virusi kwa jina la Hanter aina ya Andes ambavyo hueneza maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu katika watu wawili waliotoka kwenye meli iliyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo. Haya yameelezwa leo bungeni na Waziri wa Afya wa nchi hiyo.

Imeelezwa kuwa, mlipuko maambukizi ya  virusi vya Hanter umetokea kwenye meli ya MV Hondius, meli ya msafara wa safari za Oceanwide, ambayo kwa sasa iko karibu na kisiwa cha Cape Verd au Cabo Verde katika Bahari ya Antlantiki ya Kati kwenye pwani ya Afrika magharibi.

Binadamu huambukizwa aina nyingine za virusi vya Hanter kwa kugusana na panya walioambukizwa au mkojo wao, kinyesi au mate.

Meli hiyo ya utalii iliondoka Argentina karibu wiki tatu zilizopita ikiwa na takriban abiria 150, wakisafiri kupitia Antaktika na maeneo mengine ya mbali kabla ya kuelekea Afrika Magharibi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema lilikuwa limeanza kuwafuatilia watu waliosafiri kwa meli hiyo kati ya kisiwa cha Saint Helena na Johannesburg na kufariki dunia baada ya kuambukizwa virusi hivyo.