Shambulio la droni la RSF lauwa raia 10 waliokuwa wakielekea harusini katikati mwa Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i139730-shambulio_la_droni_la_rsf_lauwa_raia_10_waliokuwa_wakielekea_harusini_katikati_mwa_sudan
Mtandao wa Madaktari wa Sudan leo umeripoti kuwa shambulio la ndege zisizo na rubani lililofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) limeua raia 10, wakiwemo wanawake watano kutoka familia moja, katikati mwa Sudan walipokuwa wakieleke harusini.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Jul 08, 2026 12:20 UTC
  • Shambulio la droni la RSF SUdan lauwa watu 10
    Shambulio la droni la RSF SUdan lauwa watu 10

Mtandao wa Madaktari wa Sudan leo umeripoti kuwa shambulio la ndege zisizo na rubani lililofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) limeua raia 10, wakiwemo wanawake watano kutoka familia moja, katikati mwa Sudan walipokuwa wakieleke harusini.

Mtandao huo umesema katika taarifa uliyoitoa leo kwamba wahanga wa hujuma hiyo walikuwa wakisafiri katika barabara ya Assadirat magharibi mwa mji wa Omdurman wakati walipolengwa na shambulio la ndege isiyo na rubani ya wanamgambo wa RSF. Ndege hiyo ilipiga gari ya raia na kusababisha kuwaka moto na kuuwa abiria wote katika gari hiyo.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umelitaja shambulio hilo la RSF kuwa ni "ukiukaji mkubwa" wa sheria za kimataifa za kibinadamu, ukisema kuwa shambulio hilo llimefanywa kwa makusudi kwa kutumia ndege isiyo na rubani kuwalenga raia wa kawaida.

Aidha umetoa wito ukitaka kushinikizwa uongozi wa RSF kuhusu kuwalenga raia kwa makusudi kinyume na sheria za kimataifa na kanuni za kibinadamu.

Sudan imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kuwania madaraka tangu mwezi Aprili 2023, jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wa RSF. Mzozo huo umesababisha mojawapo ya majanga mabaya zaidi ya binadamu duniani, na kusababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu pamoja na kupelekea karibu watu milioni 13 kuwa wakimbizi.