Tunisia yaopoa miili ya wahamiaji wanne baada ya boti kuzama karibu na pwani ya nchi hiyo
-
Miili minne ya wahamiaji wasio na vibali yaopolewa katika pwani ya Tunisia
Mamlaka za Tunisia imepata miili ya wahamiaji wanne wasio na vibali karibu na pwani ya Ben Guerdane, kusini-mashariki mwa nchi hiyo, baada ya boti iliyokuwa imebeba watu 15 kupinduka. Haya yameelezwa jana na Shirika la Kutetea Haki za Binadamu.
Mostafa Abdelkebir, Mkuu wa Shirika la la Haki za Binadamu la Tunisia aliambia shirika la habari la Anadolu kwamba wahamiaji 15 waliondoka Jumatano kutoka pwani ya maeneo ya Ben Guerdane na Zarzis, katika mji wa Medenine unaopatikana kusini-mashariki mwa nchi hiyo katika harakati za kuelekea Italia na kisha boti yao kupinduka na kuzama.
Ameongeza kuwa askari usalama walifanikiwa kumwokoa mhamiaji mmoja miongoni mwa waliopotea siku ya Ijumaa, huku shughuli za kuwatafuta watu wengine waliosalia zikiendelea.
Tunisia ni kituo kikuu cha kuanzia safari kinachotumiwa na wahamiaji wasiofuata taratibu rasmi na wasio na vibali wanaotaka kuvuka Bahari ya Mediterania kuelekea Ulaya.
Hata hivyo, majaribio ya uhamiaji yamepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, huku mamlaka za Tunisia zikiongeza kasi ya kudhibiti uhamiaji haramu na kuimarisha ulinzi katika mipaka ya baharini.