Kamati ya mazungumzo ya Libya yatia saini rasimu ya makubaliano ili kurekebisha muundo wa tume ya uchaguzi
-
Kutiwa saini rasimu ya makubaliano ya kurekebisha muundo ya tume ya uchaguzi ya Libya
Kamati ndogo ya Mazungumzo ya Libya ya '4+4' jana Jumapili ilitangaza kuhusu kusainiwa rasimu ya makubaliano ya mwisho kwa lengo la kuifanyia marekebisho ya kimuundo Tume Kuu ya ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo na kupitia upya sheria za uchaguzi.
Makubaliano hayo yalisainiwa katika hafla rasmi iliyofanyika makao makuu ya Ujumbe wa Usaidizi waUmoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya huko Tripoli.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya 4+4, wakiwemo mabalozi kadhaa, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Baraza Kuu la Serikali, pamoja na mwakilishi wa Baraza la Uongozi la la Libya.
Makubaliano hayo yanaelekeza kurekebishwa muundo wa bodi ya Tume Kuu ya Taifa ya Uchaguzi ambapo Dhaou Ibrahim Attia ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa bodi ya tume hiyo, na Sana al-Lishani kuwa Naibu wake.
Makubaliano hayo ya karibuni ni sehemu ya juhudi zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa za kutayarisha mazingira ya kufanyika uchaguzi huko Libya ili kuhitimisha mgawanyiko wa kisiasa nchini humo kati ya tawala mbili hasimu: Yaani Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoongozwa na Abdul Hamid Dbeibeh mjini Tripoli, inayotawala magharibi mwa Libya; na serikali yenye makao yake mashariki inayoongozwa na Osama Hammad—ambaye aliteuliwa na Baraza la Wawakilishi mapema mwaka wa 2022 serikali ambayo inasimamia masuala ya mashariki mwa Libya pamoja na sehemu kubwa ya kusini mwa nchi hiyo.