Jun 01, 2023 08:54 UTC
  • Rais Yoweri Museveni
    Rais Yoweri Museveni

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amekataa wito wa nchi za Magharibi wa kufuta sheria dhidi ya ushoga iliyopasishwa na Bunge la nchi hiyo na kuidhinishwa na yeye mwenyewe.

Rais wa Uganda amesema katika taarifa yake iliyotolewa baada ya mkutano na wanachama wa chama chake cha National Resistance Movement kwamba: "Utiaji saini wa muswada wa kupinga ndoa za watu wenye jinsia moja umekamilika, hakuna mtu atakabadilisha hatua yetu. Tunapaswa kuwa tayari kwa mapambano."

Museveni amesisitiza kuwa kutiwa saini kwa sheria hiyo ni makubaliano yaliyokamilika. 

"NRM haijawahi kuwa na lugha mbili, tunachokuambia mchana ndicho tutakuambia usiku," aliongeza Rais Yoweri Museveni.

Rais Yowerii Museveni

Matamshi hayo ya Rais wa Uganda yametolewa kujibu upinzani wa mashirika eti ya kutetea haki za binadamu na nchi za Magharibi zinazohamasisha ushoga na ndoa baina ya watu wenye jinsia moja. 

Siku chache zilizopita Rais wa Marekani, Joe Biden, aliikosoa sheria hiyo akiitaja kuwa ni "ukiukaji wa kutisha wa haki za binadamu" na akataka ifutwe. Biden ametishia kuiwekea viikwazo Uganda kwa sababu ya kupiga marufuku ubaradhuli na uchafu huo wa kimaadili. 

Sheria hiyo iliyotiwa saini na Rais Museveni inatoa adhabu kali kwa wahalifu wanaopatikakana na hatia ya kujihusisha na vitendo vichafu cha ushoga na wale wanaopatikana na hatia ubakaji wa mtu aliye na umri wa chini ya miaka 18, au wale wanaoambukiza wenzao ugonjwa usiopona ikiwa ni pamoja na virusi vya Ukimwi.