Mamdani ala kiapo kwa Qur'ani, sasa rasmi ni Meya wa New York
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i134990-mamdani_ala_kiapo_kwa_qur'ani_sasa_rasmi_ni_meya_wa_new_york
Zohran Mamdani leo amekuwa Meya wa kwanza wa Jiji kubwa zaidi la Marekani la New York baada ya kuula kiapo akitumia kitabu cha Qur'ani.
(last modified 2026-01-01T05:07:46+00:00 )
Jan 01, 2026 05:06 UTC
  • Mamdani ala kiapo kwa Qur'ani, sasa rasmi ni Meya wa New York
    Mamdani ala kiapo kwa Qur'ani, sasa rasmi ni Meya wa New York

Zohran Mamdani leo amekuwa Meya wa kwanza wa Jiji kubwa zaidi la Marekani la New York baada ya kuula kiapo akitumia kitabu cha Qur'ani.

Mamdani, ambaye ni Meya wa kwanza Muislamu wa Jiji la New York mwenye asili ya Asia Kusini na aliyezaliwa barani Afrika ametumia Msahafu wa babu yake wa tangu miaka 200 iliyopita ulioazimwa kutoka Maktaba ya Umma ya New York (NYPL) kwa ajili ya hafla ya faragha ya kuapishwa iliyofanyika katika kituo cha treni ya chini ya ardhi kilichokuwa hakitumiki chini ya eneo la Times Square.