Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Oman wasisitiza kuimarisha uhusiano wa nchi zao
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i135344-mawaziri_wa_mashauri_ya_kigeni_wa_iran_na_oman_wasisitiza_kuimarisha_uhusiano_wa_nchi_zao
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman wamesisitiza azma thabiti ya nchi zao ya kuimarisha na kupanua uhusiano wa nchi zao katika nyanja mbalimbali.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jan 10, 2026 23:08 UTC
  • Mazungumzo ya Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Oman
    Mazungumzo ya Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Oman

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman wamesisitiza azma thabiti ya nchi zao ya kuimarisha na kupanua uhusiano wa nchi zao katika nyanja mbalimbali.

Sayyid Badr bin Hamad Al Busaidi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Oman ambaye yuko hapa Tehran kwa ziara rasmi, leo amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mazungumzo baina ya mawaziri hao yamefanyika katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Pamoja na masuala mengine, Mawaziri wa Mashauri ya Kigeniw a Iran na Oman wamejadili uhusiano wa pande mbili na baadhi ya masuala ya kikanda na kimataifa.

Aidha wamebadilishana Mawazo kuhusu nyanja mbalimbali za ushirikiano kati ya Iran na Oman na njia za kuimarisha zaidi mahusiano hayo.