Umoja wa Mataifa: Watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i135346-umoja_wa_mataifa_watu_milioni_30_nchini_sudan_wanahitajia_msaada_wa_haraka
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka wa kibinadamu.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jan 10, 2026 23:10 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka
    Umoja wa Mataifa: Watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watu milioni 30 nchini Sudan wanahitajia msaada wa haraka wa kibinadamu.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, vita na mzozo katika nchi ya Sudan umeingia katika siku yake ya 1,000, na zaidi ya Wasudan milioni 30 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema: raia wanapitia vurugu mbaya na kulazimishwa kuhama, wakiishi katika hali mbaya. Wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na dawa, na wanakabiliwa na magonjwa mengi.

Sehemu nyingine ya ripoti hiyo inasema: Misaada ya kibinadamu kwa kiasi kikubwa haitoshi kutokana na ugumu wa upatikanaji.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema, kukosekana kwa matarajio yoyote ya suluhisho la kisiasa na uzito wa hali hiyo kunatokana na ukubwa wa vurugu kama vile ukosefu wa msaada mkubwa wa kimataifa.