Wananchi wa Korea Kusini waandamana kuunga mkono Palestina na kuilaani Israel
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i135348-wananchi_wa_korea_kusini_waandamana_kuunga_mkono_palestina_na_kuilaani_israel
Raia wa Korea Kusini wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Seoul na kutangaza mshikamano wao na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na kulaani sera za utawala haramu wa Israel.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jan 10, 2026 23:12 UTC
  • Wananchi wa Korea Kusini waandamana kuunga mkono Palestina na kuilaani Israel
    Wananchi wa Korea Kusini waandamana kuunga mkono Palestina na kuilaani Israel

Raia wa Korea Kusini wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Seoul na kutangaza mshikamano wao na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na kulaani sera za utawala haramu wa Israel.

Waaandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wametoa mwito wa kupelekwa bila kuzuiizi misaada ya kibinadamu kwa wananchi wa Ukanda wa Gaza wanaokabiliwa na mzingiro wa utawala haramu wa Israel.

Waandamanaji hao mbali na kubeba mabango na maberamu yaliyokuwa na jumbe mbalimbali za kuunga mkono Palestina wametoa mwito wa kushughulikiwa haraka maafa ya kibinadamu yanayolikabili eneo la Ukanda wa Gaza.

Kadhalika waaandamanaji hao wamekosea uzembe wa jamii ya kimataifa na kuzitaka asasi za kimataifa kuchukua hatua za maana na za haraka kukomesha hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda huo.