Walowezi sita wa Israel waangamizwa na makumi wajeruhiwa karibu na Tel Aviv + Video + Picha
Takriban walowezi sita wa utawala wa Kizayuni wameangamizwa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika operesheni ya kulipiza kisasi ya lori kwenye kituo cha mabasi karibu na makutano ya barabara ya Glilot kaskazini mwa Tel Aviv. Eneo lilipotokea tukio hilo kitovu cha kibiashara cha mji mkuu huo wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kitengo cha Huduma ya Dharura cha Magen David Adom (MDA) kimethibitisha habari hiyiio na kusema kuwa operesheni hiyo ilifanyika jana Jumapili baada ya lori kugonga kituo cha basi huko Ramat Hasharon.
"Walowezi 6 wa Kizayuni wameangamizwa na wengi 50 wamejeruhiwa," imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa, walowezi 35 wamelazwa hospitalini kufuatia tukio hilo. Sita kati ya walowezi waliowahishwa hospitalini wana hali mbaya, watano wana hali ya hali ya wastani, 20 wamejeruhiwa kidogo.
Taarifa za awali zilisema kuwa, zaidi ya walowezi 50 wamejeruhiwa katika tukio hilo, kati yao 10 wakiwa katika hali mbaya na baadhi yao walikuwa bado wamekwama chini ya gari hilo. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, wanajeshi 20 wa Israel ni miongoni mwa walowezi 50 waliojeruhiwa.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali wa polisi, basi lilikuwa limesimama kwenye kituo ili kushusha abiria ghafla lori liliingia kwenye kituo na kuwakanyaga watu waliokuwa hapo.
Duru nyingine za habari za utawala wa Kizayuni zimetangaza kuwa, wote waliojreuhiwa ni askari wa kikosi cha 8200 cha Glilot cha utawala wa Kizayuni.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba dereva wa lori alikuwa mkazi wa mji wa Kiarabu wa Qalansawe na kubainisha kuwa alitoka kwenye lori baada ya kugonga lori akiwa na kisu mikononi mwake. Glilot iko karibu na eneo la Herzliya lenye makao makuu ya Shirika la Kijasusi la israel Mossad pamoja na vitengo kadhaa vya kijasusi vya jeshi la utawala wa Kizayuni.
Hapa chini tumeweka baadhi ya picha na video kuhusu tukio hilo: