May 14, 2024 05:57 UTC
  • Amir Abdollahian: Kuendelea uingiliaji wa Marekani nchini Afghanistan kunatatiza zaidi hali ya nchi hiyo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa kuendelea uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya Afghanistan kutafanya hali ya mambo ya nchi hiyo kuwa ngumu zaidi.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Hossein Amir Abdollahian amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatilia maanani na kufuatilia kwa karibu na kwa makini uthabiti, usalama na matukio ya Afghanistan na kuunga mkono mchango wa Umoja wa Mataifa katika kuwasaidia wananchi wa nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza haya katika mazungumzo na Bi Roza Atenbayeva, Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan. 

Amir Abdolllahian amesema kuwa wiki mbili zilizopita Umoja wa Mataifa umetekeleza hatua chanya huko Afghanistan na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono kuendelea shughuli za kibinadamu huko Afghanistan. 

Mkuu wa chombo cha diplomasia cha Iran pia ameashiria namna Iran ilivyowakaribisha na kuwapa hifadhi mamilioni ya wakimbizi wa Kiafghani na kuutaka Umoja wa Mataifa uzingatie pakubwa suala hili. 

Wakimbizi wa Kiafghani waliopewa hifadhi nchini Iran 

Bi Atenbayeva pia ameashiria matukio ya karbuni na masuala ya Afghanistan na kikao kijacho cha Doha 3 huko Qatar na akapongeza mapokezi mazuru ya serikali na wananchi wa Iran mkabala wa raia wa Kiafghani na juhudi zilizotekelezwa kwa ajili ya kuboresha hali za raia hao. 

Tags