May 20, 2024 11:57 UTC
  • Mkuu wa Kitengo cha Ng'ambo cha IRIB atuma rambirambi kufuatia kufa shahidi Rais Raisi

Mkuu wa Kitengo cha Ng'ambo cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) ametoa salamu za rambirambi kufuatia kufa shahidi Rais wa Iran Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta akiwa pamoja na maafisa wengine waandamizi.

Katika ujumbe wake siku ya Jumatatu, Dkt. Ahmad Norouzi amewataja mashahidi hao kama "waja watakasifu" ambao walijitolea kuwahudumia wananchi.

Amebainisha kuwa si Iran pekee bali ulimwengu mzima wa Kiislamu na wananchi madhlumu na wasio na sauti wa Palestina walionufaika na baraka za mashahidi wa tukio hilo la kusikitisha, wanaomboleza.

Katika ajali hiyo ya helikopta iliyotokana na hali mbaya ya hewa, Rais Seyed Ebrahim Raisi na walioandamana naye, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, Ayatullah Seyed Mohammad Ali Al-Hashem, Imamu wa Ijumaa wa Tabriz, Malik Rahmati, Gavana wa Azerbaijan Mashariki, pamoja na timu ya walinzi wa rais na marubani wamekufa shahidi.

Dkt. Norouzi, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Press TV, amesema wananchi wa Iran, watu duniani kote wamewaombea dua wapiganaji hao wa kweli ambao walikuwa katika njia ya mapambano na muqawama ya Jamhuru ya Kiislamu dhidi ya madola ya kibeberu yenye kiburi.