May 21, 2024 12:32 UTC
  • Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran asisitiza kusitishwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametilia mkazo kusitishwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina.

Ali Bagheri Kani Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezungumza kwa simu na Hakan Fidan Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki na kumshukuru kwa salamu za pole na taazia alizotoa kwa nchi hii kufuatia kufa shahidi Rais na Waziri wa Mambo ya Nje katika ajali ya helikopta; na kutaka kuendelezwa ushirikiano kati ya Uturuki na Iran ili kusitishwa mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanya na utawala muuaji wa Israel. Kaimu Waziri wa  Mambo ya Nje wa Iran ametaka pia kuungwa mkono wananchi madhulumu wa Palestina. 

Hakan Fidan pia kwa mara nyingine tena ametoa mkono wa pole na kusema serikali na wananchi wa Uturuki wamekuwa na wataendelea kusimama pamoja na serikali na taifa la Iran. 

Katika upande mwingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezungumza pia kwa simu na Ayman Safadi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan na kuashiria matukio ya sasa huko Palestina na Ukanda wa Gaza; na kusisitiza kuhusu umuhimu wa kutekelezwa juhudi za pamoja kati ya Iran na Jordan na nchi nyingine za Kiislamu ili kusitisha vita dhidi ya Gaza haraka iwezekanavyo, kikamilifu na bila ya masharti yoyote. 

Ayman Safadi na Bagheri Kani 

Katika mazungumzo hayo, Ayman Safadi Naibu Waziri Mkuu na ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan ametoa mkono wa pole kufuatia kufa shahidi Rais Sayyid Ebrahim Raisi na ujumbe aliokuwa amefuatana nao na kusema: Jordan inataka kuendelezwa mashauriano kati ya nchi hiyo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili kudhamini maslahi ya nchi mbili na kusaidia kurejesha amani na uthabiti katika Mashariki ya Kati.  

Tags