Jun 13, 2024 03:06 UTC
  • Jalili: Sera ya mashinikizo ya juu ya US ilifeli katika urais wa Shahidi Raisi

Mgombea wa uchaguzi wa rais nchini Iran amesema marehemu Shahidi Rais Ebrahim Raisi alifanikiwa kusambaratisha sera ya mashinikizo ya juu zaidi ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Saeid Jalili, mmoja wa wagombea wa urais nchini Iran alisema hayo jana Jumatano katika mkutano wa kampeni za uchaguzi katika mji wa Birjand, mashariki ya nchi na kuongeza kuwa, Sayyid Raisi alifungamana na sera ya nje ambayo ilipelekea Iran kuwa na uhusiano mzuri na nchi nyingi duniani, isipokuwa nchi chache za Magharibi.

Wagombea wa kiti cha rais nchini Iran wameanza kunadi sera na kubainisha mipango yao kuhusu ustawi wa nchi huku kampeni za uchaguzi zikianza kushika kasi.

Wagombea sita akiwemo Jalili, na Spika wa Bunge la Iran, Muhammad Baqer Qalibaf wameidhinishwa na Baraza la Kulinda Katiba kuwania urais katika uchaguzi wa rais wa kabla ya wakati uliopangwa kufanyika Juni 28.

Mkutano wa kampeni Iran

Kura hiyo iliitishwa baada ya Rais Ebrahim Raisi kufa shahidi akiwa na watu wengine saba mnamo Mei 19, wakati helikopta iliyokuwa imewabeba ilipoanguka katika mkoa wa Azerbaija Mashariki, eneo la milima la kaskazini-magharibi mwa Iran huku kukiwa na hali ya ukungu. 

Jalili ambaye ni mjumbe mkuu wa zamani wa mazungumzo ya nyuklia ya Iran akiashiria kukiri maafisa wa Marekani kwamba sera yao ya mashinikizo ya juu dhidi ya Iran imeshindwa amesisitiza kuwa, utawala wa Shahidi Raisi ulifanikiwa kuvunja sera hiyo ya vikwazo vya kikatili ya Washington dhidi ya Wairani.

Tags