Aug 10, 2024 02:34 UTC
  • Kan'ani: Kama serikali za Kiislamu zingeiunga mkono Palestina kivitendo, watu wa Gaza wasingechinjwa

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa kuzembea kwa (baadhi) serikali za Kiislamu katika kuitetea Palestina na kusisitiza kuwa, lau serikali za Kiislamu zingeiunga mkono kivitendo Palestina, watu wa Gaza wasingechinjwa namna hii

Nasser Kan'ani Chafi amesema hayo katika ujuumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X na kuonyesha kusoneshwa na hatua ya tawala za Kiislamu ya kutotoa himaya na uungaji mkono wa dhati na wa kivitendo kwa wananchi madhulumu wa Palestina.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa mataifa ya Kiislamu kuliunga mkono taifa la Palestina ambalo kwa sasa linapatia wakati mgumu sana kutokana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko katiika ukanda wa Gaza.

Zaidi ya Wapalestina 40,000 wameuawa shahidi tangu Israel ianzishe hujuma ya kinyama dhidi ya Gaza Oktoba mwaka jana (2023)

 

Aidha kabla ya hapo Kan'ani Chafi alituma ujumbe mwingine katika ukurasa wake wa mtandao wa kijami wa X na kueleza kwamba, lau kama jamii ya kimataifa ingetekeleza vizuri majukumu yake, leo hii tusingelishuhudia miezi 10 wa jinai, ukatili, maangamizi ya kizazi na mauaji ya halaiki ya wanawake na watoto wadogo yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Kadhalika amesema, dunia inapasa kuelewa kuwa, genge la wahalifu na watenda jinai linaloongozwa na Benjamin Netanyahu ndani ya serikali ya utawala wa Kizayuni wa Israel litaendelea kukaidi kuheshimu sheria za kimataifa maadamu hakutachukuliwa hatua kali za kivitendo za kutiwa adabu Israel na kulazimishwa iheshimu sheria hizo.