Sep 18, 2024 11:47 UTC
  • Muhammad Qalibaf
    Muhammad Qalibaf

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amekutaja kuuwa watu wasio na hatia kuwa ni sehemu isiyotenganishika ya tabia na hulka ya kutenda maovu ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la Habari la Iran (IRNA) limeripoti kuwa, Muhammad Bagher Qalibaf ameashiria matukio ya jana huko Lebanon na kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba: "Ugaidi na kuwauwa watu wasio na hatia ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya tabia ya uovu ya utawala wa Kizayuni. Utawala huu hautaacha kutekeleza mauaji ya kimbari madhali bado upo." 

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ameongeza kuwa: "Tunalaani vikali hujuma ya kigaidi iliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Lebanon na tunatangaza mshikamano wetu na wahanga wa hjuma hiyo; tuko pamoja na wananchi wa Lebanon kama ilivyokuwa huko nyuma."  

Ripoti zilizotufikia hadi sasa zinasema watu 11 wameuawa shahidi akiwemo binti mmoja mdogo, na raia wengine wa Lebanon elfu tatu wamejeruhiwa katika milipuko ya jana ya  vifaa vya mawasiliano kwa jina la "Pager" katika maeneo tofauti ya Lebanon, hususan katika mji mkuu wa nchi hiyo, Beirut. 

Naye Firass Abiad, Kaimu Waziri wa Afya wa Lebanon amethibitisha kuwa watu wasiopungua 11 wameuawa akiwemo binti aliyekuwa na umri wa miaka 8 katika hujuma hiyo ya kigaidi ya Israel.

Amesema, watu zaidi ya 200 wako katika hali ambayo baada ya kujeruhiwa katika milipuko ya vifaa vya Pager; na kwamba aghalabu ya waliojeruhiwa wamepata majeraha makubwa usoni, mikononi na tumboni. 

Hujuma ya kigaidi ya vifaa vya Pager iliyofanywa na Israel huko Lebanon 

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetoa taarifa tofauti na kuitaja Israel kuwa imehusika na milipuko hiyo ya vifaa vya Pager, na kusema bila shaka italipiza kisasi kwa hujuma hiyo.  

Tags