Ayatullah Khamenei: Njia pekee ya kumaliza vita Asia Magharibi ni kupungua uovu wa Marekani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, chimbuko la matatizo ya eneo la Asia Magharibi ni mataifa kama Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zinazodai kwa uwongo kwamba, zinataka amani na utulivu.
Ayatullahh Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo alipokutana na mamia ya watu wenye vipaji vya elimu hapa nchini na waliong'ara katika mashindano ya olimpiadi na mitihani ya kuingia katika vyuo vikuu na kusisitiza ulazima wa kunufaika na watu wenye vipaji katika sekta mbalimbali na ulazima wa kuandaliwa mazingira ili watu wenye vipawa wawe na taathira katika masuala mbalimbali ya nchi.
Akizungumzia matukio ya Asia Magharibi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, njia pekee ya kumaliza mizozo na vita katika eneo hili ni kupunguza maovu ya nchi hizi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameuchukulia uchochezi wa Saddam wa kuishambulia Iran na siku za machungu na magumu kuwa ni mfano wa wazi wa uanzishaji vita wa Marekani na Magharibi katika eneo na kuongeza: Huba na upendo uliopo hivi sasa kati ya nchi mbili za Iran na Iraq, ambao kilele chake ni katika matembezi makubwa ya Arubaini ya Imamu Hussein (as) ni mfano wa wazi unaoonyesha kuwa sababu kuu ya matatizo ya eneo hili ni wadai bandia wa amani, ambao kkwa tawfiq ya Mwenyezi Mungu na juhudi kubwa za taifa la Iran na kwa msaada wa miongozo ya Mapinduzi ya Kiislamu na ushirikiano wa mataifa mengine maovu yao yatapungua katika eneo.