Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini Lebanon ni 'hatua ya kijasiri'
(last modified Sat, 05 Oct 2024 06:11:19 GMT )
Oct 05, 2024 06:11 UTC
  • Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini Lebanon ni 'hatua ya kijasiri'

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon Mojtaba Amani amesema safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi nchini Lebanon ilikuwa "safari ya kijasiri na yenye kuonyesha nguvu."

Katika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa X siku ya Ijumaa, Amani amesema: "safari ya Araghchi nchini Lebanon itakuwa na "matokeo muhimu ya kikanda."

Aidha amesema: "Iran daima imeonyesha kuwa itasimama na Lebanon katika hali ngumu."

Balozi Amani ameendelea kusema kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haitaruhusu hatima ya eneo kubadilishwa na Marekani na utawala haramu ya Kizayuni." Ameendelea kusema kuwa: "Mustakabali utaamuliwa na nchi za kanda hii chini ya uongozi wa muqawama."

Araghchi alifanya ziara ya kushtukkiza katika mji mkuu wa Lebanon Beirut siku ya Ijumaa.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghae aliandika kaktika ukurasa wake wa X siku ya Ijumaa kwamba: ".Nimetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beirut. Ujumbe wetu ukiongozwa na Waziri Araghchi ukiambatana na wabunge wawili na Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran utakutana na maafisa wa ngazi za juu wa Lebanon."

Alisema ndege iliyokuwa imembeba Waziri Aragchi ilikuwa na kifurushi cha tani 10 za vyakula na dawa ikiwa ni sehemu ya usaidizi wa kibinadamu wa Iran kwa Lebanon.

Araghchi alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa muda wa Lebanon, Najib Mikati, na kusisitiza uungaji mkono usioyumba wa Iran kwa Lebanon katika kukabiliana na ukatili wa utawala ghasibu wa Israel.