Tamasha la Asubuhi: Sauti ya Muqawama dhidi ya ubeberu wa kimataifa, linaendelea Tehran
(last modified Wed, 07 May 2025 06:37:01 GMT )
May 07, 2025 06:37 UTC
  • Tamasha la Asubuhi: Sauti ya Muqawama dhidi ya ubeberu wa kimataifa, linaendelea Tehran

Tamasha la tatu la vyombo vya habari la "Sobh", (Asubuhi) kwa ajili ya kuwaenzi watu mashuhuri wanaopinga ubeberu, kuanzia wabunge wa zamani wa mabunge ya Ulaya na Uingereza hadi mwandishi wa habari wa Palestina kutoka Gaza, linaendelea kupaza sauti ya mapambano na Muqawama dhidi ya ukandamizaji wa kimataifa.

Tamasha hilo ambalo lilianza mjini Tehran likihudhuriwa na Peyman Jebelli, Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Iran (IRIB), Ahmad Norouzi, Mkurugenzi wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo cha IRIB, na kundi la watu mashuhuri wanaopinga ubeberu wa kimataifa kutoka kote duniani.

Tamasha hilo ambalo lilianza Mei 3 na linaendelea hadi 8 Mei, limekabidhi tuzo maalumu kwa Clare Daly na Mick Wallace (wabunge wa zamani wa Bunge la Ulaya), George Galloway (mbunge wa zamani wa Uingereza), Ahmed Sahmood (mwandishi wa habari Mpalestina wa Televisheni ya Al-Alam katika Ukanda wa Gaza), na Masoud Najabati (msanii wa picha wa Iran) kwa juhudi zao za kuunga mkono Muqawama na mapambano dhidi ya dhulma na ukandamizaji.

Washindi wa Tuzo ya Tamasha la Tatu la Sobh

Katika hotuba yake kwenye tamasha hilo, Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Iran (IRIB) amezungumzia nafasi ya vyombo vya habari huru katika kuakisi sauti za wanyonge na kusimama katika "upande wa kulia wa historia" na kuwaenzi mashahidi wa Kambi ya Muqawama kama Ismail Haniyeh, Sayyid Hassan Nasrullah na Yahya Sinwar.

Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Iran ameyakosoa madola ya kibeberu ambayo yanawashambulia watoto wa Gaza kwa "silaha na mabomu," na kusema, fahari ya Muqawama ni kusimama kwake kidete dhidi ya ukandamizaji na na fahari ya kupanuka harakati ya kupinga Uzayuni kutoka Mashariki hadi Magharibi mwa dunia.

Peyman Jebelli ameashiria ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kote duniani na kuyataja maandamano ya kupinga ubeberu kuwa ni sehemu ya harakati ya Muqawama. Amesisitiza wajibu wa vyombo vya habari kuvunja "duara ya kimya" na kubakisha hai historia.

Peyman Jebelli

Kwa upande wake, Ahmed Nourouzi, Mkurugenzi wa Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo cha IRIB amesema kuwa mahudhurio ya watu mashuhuri na wa kimataifa katika tamasha hilo ni fahari kwa mwenyeji, na amesifu ujasiri wa waandishi wa habari wa Televisheni za Al-Alam na Press TV katika kuandika habari kuhusu jinai za Wazayuni huko Gaza na Lebanon.

Nourouzi ameashiria takwimuu za kutisha za kuuawa shahidi asilimia 8 ya wakazi wa Gaza hususan wanawake na watoto katika mashambulizi ya Wazayuni na kupongeza msaada wa Iran kwa Palestina.

Pia ametuma salamu maalumu kwa roho za waandishi wa habari 200 waliouawa shahidi katika njia ya kusema ukweli na haki.