Iran yatungua ndege 2 za kivita za Israel za F-35, yamkamata rubani
(last modified Sat, 14 Jun 2025 07:05:35 GMT )
Jun 14, 2025 07:05 UTC
  • Iran yatungua ndege 2 za kivita za Israel za F-35, yamkamata rubani

Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimefanikiwa kutungua na kuteketeza ndege mbili za kivita za Israel aina ya F-35, na idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani. Iran imekuwa nchi ya kwanza duniani kuweza kutungua ndege ya kijeshi ya F-35.

Ndege hizo za kisasa na zenye thamani kubwa za Israel zilitunguliwa usiku wa kuamkia leo Jumamosi. Kwa mujibu wa ripoti, rubani wa mojawapo ya ndege hizo za kivita ambaye ni mwanamke amekamatwa.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeapa kuendelea kutoa majibu makali na mazito kwa vitendo vya uchokozi vya utawala haramu wa Israel.

Utawala wa Israel ulishambulia vitongoji kadhaa vya makazi ya watu mjini Tehran na katika maeneo mengine ya Iran usiku wa kuamkia jana Ijumaa.

Vikosi vya ulinzi wa anga vimefanikiwa kutungua makombora ya maadui yaliyorushwa na utawala wa Kizayuni katika anga ya mji mkuu wa Iran, Tehran.

Wakati wa operesheni hiyo iliyotokea katika maeneo ya kati na kusini mwa Tehran, vikosi vya ulinzi wa anga vya Jamhuri ya Kiislamu vilifanikiwa kuzima makombora yote ya Wazayuni kabla ya kupiga shabaha zilizokusudiwa.

Usiku wa kuamkia leo, Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vilianza kutekeleza wimbi la mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel, ili kulipiza kisasi kufuatia hujuma za utawala huo wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya Iran.