Spika Qalibaf: Utawala wa Kizayuni umechafua tena mikono yake kwa jinai mpya kwa idhini ya Marekani
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amebainisha kuwa, utawala haramu wa umechafua mikono yake michafu kwa jinai mpya kwa idhini ya Marekani na kueleza kuwa, "watu wa Iran, wa kila kabila na mirengo tofauti ya kisiasa, wameungana na kuwa kitu kimoja dhidi ya adui katili, na bila shaka walimwengu watashuhudia adhama ya Iran na Wairani."
"Mohammad Baqer Qalibaf," Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu amesema hayo katika hotuba yake ya utangulizi katika kikao cha jana (Jumatatu) cha Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na kulaani hujuma na uchokozi wa utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya Jamhuri yaa Kiislamu ya Iran.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kwamba, "Utawala wa kibaguzi na kijinai wa Kizayuni, kwa uungaji mkono na idhini ya serikali ya Marekani, umechafua mikono yake michafu yenye kutapakaa damu kwa jinai mpya katika nchi yetu tunayoipenda, umeshambulia kwa woga maeneo ya makazi, hospitali, vifaa vya kutoa msaada, na miundombinu ya kiraia, na kuua kundi la wanawake, watoto na raia madhulumu majumbani mwao na kwa mara nyingine tena umeweka wazi hali yake ya ubaya na ukatili ambayo umezoea ya miaka themanini ya umwagaji damu.
Spika wa Bunge la Iran ameongeza kuwa: Jinamizi la usiku uliopita wa Wazayuni na mwali wa moto uliozingukia roho za wahusika na makamanda wa jinai za utawala wa Kizayuni zitaendelea hadi pale mchokozi huyo atakapotubia na kuadhibiwa; wana wa Iran watatia giza siku zenu na mtakuwa masikini na dunia itatazama masaibu yenu.