Operesheni ya kijeshi ya Iran ya Ahadi ya Kweli-3 yasababisha uharibifu mkubwa Tel Aviv na Haifa
(last modified Sun, 22 Jun 2025 15:03:31 GMT )
Jun 22, 2025 15:03 UTC
  • Operesheni ya kijeshi ya Iran ya Ahadi ya Kweli-3 yasababisha uharibifu mkubwa Tel Aviv na Haifa

Wimbi jipya la mashambulio ya makombora ya Iran ya operesheni ya Ahadi ya Kweli-3 limesababisha uharibifu mkubwa katika miji ya Tel Aviv na Haifa.

Redio ya Jeshi la Israel imekiri kutokea mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Iran dhidi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) na kutangaza kuwa mawimbi mawili ya mashambulizi ya makombora yalirushwa kutoka Iran kuelekea Israel.

Redio ya Jeshi la Israel pia imeongeza kuwa: Wazayuni 20 wamenasa chini ya vifusi kutokana na shambulio la kombora la Iran huko "Nes Ziona" kusini mwa Tel Aviv.

Vyombo vya habari vya Israel vinaripoti kwamba ilikuwa vigumu kufikiria uharibifu uliosababishwa na jengo la zamani la treni huko Ramat Aviv, kaskazini mwa Tel Aviv. Polisi wa Israel pia wamewataka Waisraeli kutosafiri katika maeneo yaliyoshambuliwa na makombora ya Iran.